Saturday, October 24, 2015

TATHIMINI,MAONI NA MAOMBI KUELEKEA KESHO -25-10-2015

Niliamini hivyo na ndio ilivyokuwa leo ni siku ambayo Vyama Vyote vya siasa vimehitisha kampeni zao na kumekuwa na utilivu na uvumilivu ndani ya wananchi wa Tanzania ,sera zimetangazwa,vijembe,mipasho,usaliti vyote vimepita nami niliamini kuwa kampeni zitaisha kwa amani na hitimisho limekuwa tulivu na hakuna dhoruba kali zilizotokea.Ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu kwa rehema zake kufikia hitimisho hilo la kampeni.Vyote vimetangaza sera zao ili kuweza kuleta maboresho kwa serikali iliyopita si CCM,CHADEMA,NCCR MAGEUZI,ACT,CHAUMA,ADL,NRA ,TLP na UPDP.Kwenye  zoezi hili naamini vyama vyote vimepata fursa nzuri za kujinadi katika hali nzuri na usalama na kuwapa wananchi wasaaa wa kusikia sera na kuzitafakari na tathimini yangu kwa hili wananchi tumeweza ni jambo la kushukuru. 

Haya yote yamefanyika ili kufikia hitimisho lake kwa upigaji wa kura utakofanyika hapo kesho 25-10-2015 ili kuwezesha kupata Rais,Wabunge na Madiwani wa kusukuma nchi yetu mbele na kupata Tanzania mpya na yenye neema tele ikikumbwa ina rasilimali nyingi za kutuwenzesha kutupa maisha bora zaidi kuanzia katika Afya,Elimu,Miuundo mbinu,Makazi,Technologia,Siasa,Utamaduni n.k. kwani naamini viongozi wote waliyasema kwa nia njema na sio kwa uroho na ubinafsi wao kwa kupata kura na kushinda.

Watanzania hatuna budi twende kupiga kura ili tuweze kupata mabadiliko naamini tena Mungu atanjoosha mkono wake na kufanya zoezi hili pia liishe kwa amani kwani naamini uchaguzi wetu utakuwa wa uhuru na haki na wale wote watakao shidwa hawana budi kukubali matokeo kwa faida ya nchi.Kinyume cha hapo twawenza kusababisha machafuko ambayo yanaweza kuharibu mifumo yetu mingi na kusababisha nchi kudumaa zaidi katika kufikia mabadiliko tuliyo yahitaji sipendi kutoa mifano ya nchi zilizo ingia katika migogoro kufuatia kutokukubaliana baada ya uchaguzi kwa Watanzania wanazijua na wamekuwa mstari wa mbele kuwapokea kama wakimbizi,tudumishe amani kwa faida ya TAIFA LETU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
By Augustine


Tokeo la picha la image of tanzania flag






0 comments:

Post a Comment