Wednesday, October 14, 2015

WATANZANIA KWA NINI TUNAMKUMBUKA HAYATI MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE?

KUZALIWA,FAMILIA NA ELIMU Mwl Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 mashariki ya Ziwa Victoria katika kijijini Butiama kati ya watoto 26 wa Mzee Nyerere Burito kipindi hicho Tanzania ikitambuliwa kama Tanganyika.Kama vijana wengine Mwalimu alifanya kazi kama za kuchunga mifugo yao.Baba(Nyerere Burito) yake alikuwa ni Chifu wa Kabila dogo la Wazanaki.Alianza shule akiwa na umri wa miaka 12 katika shule ya msingi Mwisenge,iliyoko Musoma mjini baada ya elimu ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki iliyoko Tabora alibatizwa na kuwa Mkatoliki,kutokana na ushupavu,akili na bidii aliyokuwa wamisionari walimsaidia na kupata elimu yake juu katika chuo kikuu cha Makekere kati ya mwaka 1943 hadi 1945 katika fani ya Ualimu.Aliporudi Tanganyika alifanya kazi kama mwalimu katika sekondari ya mtakatifu Maria mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda Edinburg huko Uskoti-Uingereza akisoma masomo ya uchumi na historia katika shahada ya uzamili.Aliporejea Tanganyika alifundisha Historia,Kingereza na Kiswahili katika shule St francis siku hizi pugu Sekondari. SAFARI YA SIASA Mwaka 1954 alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika. Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960 WAZIRI WA TANGANYIKA HURU. UHURU NA UONGOZI WA TANGANYIKA Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba 1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah. Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na chama tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza. KUNG'ATUKA NA KIFO Nyerere aliendelea kuongoza taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi wengi.Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin W.Mkapa kama mgombea wa urais mwaka 1995 ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi MAISHA BAADA YA KUSTAAFU UONGOZI Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi KIFO Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas mjini London Uingereza baada ya kupambana na kansa ya damu KABURI ALIPOZIKWA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE. MAMBO YAKE YA KUKUMBUKWA Nyerere alikuwa mstari wa mbele katika kulikomboa bara la Africa mfano South Africa,Namibia,Angola,Msumbiji n.k ,Nyerere ameandika vitabu vingi ambavyo kama vijana wa leo wangekuwa na moralali ya kusoma tungeweza kuchota mambo mazuri na kumuenzi. Nyerere amekuwa mfano mzuri katika kupambana na rushwa na kuleta usawa baina ya Tanzania huku akiamini katika ujamaa. Hotuba zake zimekuwa na uwezo wa kuishi mpaka leo zikiwa na maneno ya kufurahisha na kufundisha Nyerere alifanikiwa katika kuunganisha nchi ya Zanzibar na Tanganyika, Katika kuleta umoja wa kitaifa,utamaduni na kudumisha lugha ya kiswahili.HUYO NDIO BABA WA TAIFA AMBAYE KILA MTANZANIA ANAAMINI HAMNA MBADALA WAKE KATIKA UONGOZI NI TAKRIBANI MIAKA 16 YA KIFO CHAKE NA MIAKA 24 YA UONGOZI HAKIKA ALIKUWA jEMBE NA KAZI ALIIFANYA.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MLAZE MAHALI PEMA PEPONI.

0 comments:

Post a Comment